KISWAHILI KIDATO CHA TATU

KIDATO CHA: TATU
                          MADA YA KWANZA: NGELI ZA MANENO
Kuzielewa Ngeli
Upatanishi wa Kisarufi katika Sentensi
Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana.
Mfano:
 1. Maji yakimwagika hayazoleki
 2. Mayai yaliyooza yananuka sana
 3. Yai lililooza linanuka sana
 4. Maji liliomwagika halizoleki
Katika mifano hii tunaona kwamba sentensi a, b na c ziko sahihi wakati sentensi d sio sahihi, hii ni kwa sababu imekiuka upatanisho wa kisarufi. Kwa maana hiyo sentensi ‘a’ ipo katika ngeli ya YA-YA na senthensi b na c zipo katika ngeli ya LI-YA. Sentesi d sio sahihi kwa sababu nomino maji haina wingi, kwa hiyo haiwezi kuingia katika ngeli ya LI-YA. Kwa msingi huu ngeli za nomino huzingatia sana upatanisho wa kisarufi.
Jedwali lifuatalo huonesha ngeli za nomino kwa misingi ya upatanisho wa kisarufi.
NGELI
UFAFANUZI
MIFANO
A-WA
Ngeli hii inahusisha majina ya viumbe hai kama vile wanyama, watu, wadudu, ndege n.k
Sungura mjanja ameumia Sungura wajanja wameumia Mkuu anawasili
LI-YA
Majina yenye kiambaisha awali li- katika umoja na ya- katika wingi huingia katika ngeli hii
Jambia la babu limepotea Majambia ya babu yamepatikana
KI-VI
Ni ngeli ya majina ya vitu visivyo hai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Pia ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo k.v, kijito, kilima
Chakula kimekwisha Vyakula vimekwisha Kijito kimekauka Vijito vimekauka
U-I
Huwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M- (umoja) na MI (wingi). Pia majina ya baadhi ya viungo vya mwili huingia humu, kewa mfano mkono, mguu, mkia n.k
Mlima umeporomoka Milima imeporomoka Mkono umevunjika Mikono imevunjika Mto huu una mamba wengi Mito hii ina mamba wengi
U-ZI
Hurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti /u/' k.v ukuta-kuta. Majina ya silabi mbili huongezewa /ny/ katika wingi. k.v ufa - nyufa
Ukuta umebomoka Kuta zimebomoka Wimbo huu unavutia Nyimbo hizi zinavutia Ufa umeonekana Nyufa zimeonekana
I-ZI
Hutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (Wingi).
Nyumba imejengwa Nyumba zimejengwa Salam imefika Salam zimefika
U-YA
Ngeli hii inajumuisha nomino ambazo zina kiambishi awali u- katika umoja na ma- katika wingi.
Ukuu umekuponza Makuu yamekuponza Unyoya unapepea Manyoya yanapepea
KU
Majina yanayotokana na vitenzi yanayoanza na ku- (vitenzi-jina)
Kusoma kwako kumekusaidia Kuchelewa kumemponza
PA/MU/KU-
Huonesha mahali
Amekaa pale palipo na wadudu wengi Amelala mule mulimojaa siafu. Amepita kule mbali
Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:
 • Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.
 • Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.
 • Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.
 • Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.
Habari zenye Upatanishi wa Kisarufi
Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:
 • Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.
 • Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.
 • Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.
 • Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.

                              MADA YA PILI: MJENGO WA TUNGO
Tungo
Tungo ni kipashio cha kisarufi kilichoundwa kwa kuunganisha pamoja vipashio vidogovidogo vilivyo chini yake. Au tungo ni neno au kikundi cha maneno ambacho hudokeza taarifa fulani ambayo huweza kuwa kamili au isiyo kamili.
Kwa maana hii, tungo hujengwa na vipashio vidogovidogo kama vile mofimu kuunda neno, neno kuunda kirai, kirai kunda kishazi na kishazi kuunda sentensi. Kama tulivyokwisha kuona hapo juu tungo huanzia neno; rejea aina za tungo.

Aina za tungo
Tungo neno: Tungo neno ni tungo ambayo huundwa na vipashio vidogo zaidi ya neno ambayo ni mofimu au fonimu. Mfano;  anacheza, kakimbia.
Tungo Kirai: ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi lakini ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu. Mfano; mtoto mzuri, kiyama chake, bondeni
Tungo kishazi:Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe.

Kirai na Uainishaji wake
Dhana ya kirai itaeleweka vizuri kwa kuzingatia sifa zake zifuatazo:
 • Kirai huwa ni kipashio cha kimuundo kisichokamilika; yaani ni kipashio kisichokuwa na muundo wa kiima – kiarifu kama zilivyo sentensi ambazo zinahusisha mtendaji wa tendo na tendo linalotendwa.
 • Kirai huainishwa kimuundo kulingana na neno kuu la kirai husika.
 • Kirai ni tungo, yaani ni aina moja wapo ya tungo, aina nyingine za tungo ni neno, kishazi na sentensi.
 • Kirai hudokeza maana, lakini maana hiyo si kamili.
 • Maneno katika kirai lazima yapangwe kimantiki kwa mpangilio unaokubalika katika sarufi ya lugha husika. Japo virai huainishwa kimuundo, huweza kutumika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi. Kirai huweza kutokea upande wowote, wa kiima au kiarifu katika sentensi. Kirai ni kikubwa kuliko neno
Kama tulivyobainisha hapo juu aina ya virai hukitwa katika aina za maneno ambazo ndizo chimbuko la mahusiano maalumu ndani ya vipashio hivyo.
 1. Kirai nomino (KN); Ni kirai ambapo neno lake kuu ni nomino. Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa kwenye nomino au mahusiano ya nomino na neno au mafungu ya maneno.
 2. Kirai kitenzi (KT); Kirai-kitenzi ni kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi au katika mahusiano ya Kitenzi na neno au mafungu mengine ya maneno. Hii ina maana kuwa neno kuu katika aina hii ya virai huwa ni kitenzi.
 3. Kirai kivumishi (KV); Kirai-kivumishi ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika kivumishi. Kwa kawaida muundo huu huwa ni wa kivumishi na neno au fungu la maneno linaloandamana nacho.
 4. Kirai Kielezi (KE); Tofauti na aina nyingine ya virai miundo ya virai vielezi haielekei kukitwa kwenye mahusiano ya lazima baina ya neno kuu (yaani kielezi) na neno au fungu la maneno linaloandamana nalo. Badala yake miuundo inayohusika hapa ni ya maneno ambayo hufanya kazi pamoja katika Lugha kama misemo, neno au maneno yanayofuata neno lililotangulia yakifafanua zaidi neno hilo.
 5. Virai viunganishi (KV); Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina ya kwa na katika, au kwenye na fungu la maneno linaloandamana nacho. Kwa maneno mengine kirai hicho ni kile ambacho neno kuu ni kiunganishi.
Tungo kishazi
Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe.
Sifa za kishazi
 • Kishazi hupatikana katika/ ndani ya sentensi.
 • Lazima kishazi kiwe na kitenzi, sehemu yoyote ya sentensi isiyo na kitenzi, haiwezi kuwa kishazi. Kishazi huru hutawaliwa na kishazi kikuu na kishazi tegemezi hutawaliwa na kishazi tegemezi.
 • Baadhi ya vishazi huweza kujitegemea kama sentensi hata vikiondoshwa katika muktadha wa sentensi kuu. Kishazi kinachoweza kujisimamia kama sentensi huitwa kishazi huru kikiwa ndani ya sentensi kuu na huitwa “sentensi sahili” kikiwa sentensi inayojitegemea.
 • Baadhi ya vishazi haviwezi kujitegemea kama sentensi ikiwa vitaondoshwa katika muktadha wa sentensi kuu.
 • Vishazi vingi, hata vishazi huru huwa na kiima dhahiri.
 • Kishazi kwa kawaida, hasa kishazi huru huwa na kitenzi kimoja kikuu.
 • Kitenzi hicho huweza kuandamana na kitenzi kisaidizi. Pia, kitenzi katika kishazi huweza kuwa kitenzi kishirikishi.
 • Kishazi hutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi.
 • Tofauti ya kishazi na sentensi ni kwamba kishazi hupatikana ndani ya sentensi lakini sentensi hujisimamia kimuundo na kimaana.Kishazi huwa na kiarifu kimoja na kiima kimoja, Lakini sentensi huweza kuwa na kiima kimoja.
Aina za vishazi
 1. Vishazi huru: Kishazi huru ni kishazi kinachotaewaliwa ka kitenzi kikuu, ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe kamili usiohitaji maelezo zaidi ya kukamilisha maana. Ni kishazi ambacho hata kikiondolewa katika muktadha wa sentensi ambamo vimejikita huweza kujitegemea kama sentensi.
 2. Vishazi tegemezi: Kishazi huru ni kishazi kinachotawaliwa ka kitenzi kisaidizi, ambacho muundo wake hukifanya kutegemea kitenzi cha kishazi huru ili kuweza kutoa ujumbe uliokusudiwa. Kishazi tegemezi peke yake hakitoi ujumbe unaojitosheleza
Sifa za Kishazi tegemezi
 • Kishazi tegegemezi hutoa maana kamili kinapoandamana na kishazi huru.
 • Kishazi tegemezi kinaweza kufutwa katika sentensi bila kuharibu maana ya sentensi nzima.
 • Kishazi tegemezi hutambulishwa na viambishi vya utegemezi
 • Vinavyoambatanishwa kwenye kitenzi.
 • Kishazi tegemezi vile vile kinaweza kutambuliwa kwa kuwepo vishazi kama vile ingawa, kwamba, ili, kwa sababu, mzizi wa amba, mofu ya masharti n.k
Aina ya vishazi tegemezi
Vishazi tegemezi vivumishi
 • Vishazi tegemezi vinavyotokea pamoja na nomino inayovumishwa.
 • Vishazi tegemezi visivyoambatana na nomino inayovumishwa
Vishazi tegemezi vielezi
 • Vishazi tegemezi vya mahali
 • Vishazi tegemezi vya wakati
 • Vishazi tegemezi vya namna au jinsi
 • Vishazi tegemezi vya masharti
 • Vishazi tegemezi vya hali, hitilafu au kasoro iliyoko katika tendo.
 • Vishazi tegemezi vya sababu/chanzo
Dhima na hadhi ya vishazi
Kishazi chaweza kuwa huru kikajitegemea chenyewe kwa kuwa na maana kamili inayojitosheleza. Lakini kuna vishazi ambavyo havijitoshelezi vyenyewe, bali hutegemea vishazi vingine. Kishazi huru kina hadhi ya sentensi (sahili). Kishazi tegemezi hakina hadhi hii, vishazi tegemezi ambavyo hutegemea vishazi vingine hushuka daraja na kuchukua dhima ya kikundi. Baadhi ya vishazi tegemezi huchukua dhima (hufanya kazi) ya kivumishi katika tungo ambayo kwa kawaida ni dhima ya kikundi au neno. Vishazi hivi huvumisha nomino katika tungo hiyo.

Ufafanuzi wa Aina za Tungo
Sentensi
Sentensi ni kifungu cha maneno kuanzia neno moja na kuendelea chenye muundo wa kiima na kiarifu na kinacholeta maana kamili.

Sifa za sentensi
Sentensi lazima iwe na mpangilio wa maneno ambao unakubalika na wazungumzaji wa lugha husika.
 • Sentensi lazima ikamilike kimaana, kimuundo na kisarufi.
 • Sentensi huwa na muundo wa kiima na kiarifu /huwa na kirai nomino na kirai kitenzi.
 • Sentensi huweza kuwa na zaidi ya kiima kimoja na kiarifu zaidi ya kimoja.
 • Sentensi inaweza kuundwa na kitenzi kikuu kimoja au zaidi.
 • Sentensi inaweza kuundwa na kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi.
 • Sentensi huonyesha hali mbalimbali, kama vile amri, ombi, mshangao, swali n.k
Muundo wa sentensi
Muundo wa sentensi kimapokeo/kikazi/kidhima
Muundo wa sentensi kimapokeo/kikazi/kidhima unakuwa na vipengele vifuatavyo:
 • Kiima: Ni sehemu katika sentensi ambayo hujaza sehemu ya mtenda au mtendwa wa jambo linaloelezwa. Katika tungo kiima hutokea kushoto mwa kitenzi.
 • Kiarifu: Ni sehemu katika sentensi inayojazwa na maneno yanayo arifu tendo lilofanywa, linapofanywa au litakapofanywa. Kiarifu ndiyo sehemu muhimu zaidi katika sentensi ambayo wakati mwengine huweza kusimama pekee, kwani wakati mwingine huchukua viwakilishi vya kiima.
Vipashio vya kiima
 • Nomino peke yake
 • Nomino, kiunganishi na nomino
 • Nomino na kivumishi
 • Kivumishi na nomino
 • Kiwakilishi peke yake
 • Kiwakilishi na kivumishi
 • Nomino na kishazi tegemezi vumishi
 • Kitenzi jina
 • Nomino na vivumishi zaidi ya kimoja
 • Kitenzi jina na nomino
 • Umbo kapa
Taarifa zitolewazo na kiarifu kuhusu kiima
 • Kiima ni nani
 • Kiima kina nini
 • Kiima hufanya nini
 • Kiima kinahisi nini
Sifa za kiarifu
 • Huwa na kitenzi na pengine huambatana na maneno mengine.
 • Kiarifu kwa kawaida huja baada ya kiima
Vipashio vya kiarifu
 • Kitenzi kikuu peke yake.
 • Kitenzi kisaidizi au vitenzi visaidizi vilivyosambamba na kitenzi kikuu.
 • Kitenzi kishirikishi na kijalizo
 • Yambwa (shamirisho)
 • Kijazalio
 • Chagizo
Sifa za chagizo
 • Chagizo kwa kawaida huwa ni kielezi au kirai husishi ambacho kinafanya kazi kama kielezi.
 • Kwa kawaida ni vipashio vya ziada. Si lazima viwepo katika sentensi ili ijisimamie.
 • Huwa cha lazima ikiwa kinafuata kitenzi kishiriki. Hali ikiwa hivyo, kinafnaya kazi kama kijalizo.
 • Hutumika kufafanua kitenzi/kivumishi /kielezi.
 • Hutumika kujaliza kiima/kama kijalizo.
Aina za sentensi
Aina za sentensi kimuundo ni pamoja na hzi zifuatazo

Sentensi sahili
Ni sentensi ambayo huundwa na kishazi huru kimoja. Sentensi ya aina hii huwa inaelezea taarifa moja tu. Mfano; Wanafuzi wanafanya mtihani; Walinzi walitaka kunizuia nisiingie ndani.
Miundo ya sentensi sahili
 • Muundo wa kitenzi kikuu peke yake. Mfano: Gari limeanguka
 • Muundo wa kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi. Mfano: Mgosiyuda alitaka (TS) nisipate (T) utajiri
 • Muundo wa vira-vitenzi vilivyokitwa katika kitenzi ‘kuwa’. Mfano: John amekuwa akiangalia TV kwa muda mrefu sana.
 • Muundo wa kitenzi shirikishi. Mfano: Kiswahili ni tunu ya Taifa
Sifa za sentensi sahili
 • Ina kiima ambacho kimetajwa wazi au kimeachwa kutajwa kwa kuwa kinaeleweka.
 • Ina kiarifu ambacho kimeundwa na kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi au kitenzi kishirikishi na kijalizo na chagizo.
 • Haifungamani na sentensi nyingine na hivi inajitosheleza kimuundo na kimaana.
Sentensi changamano
Hii ni sentensi yenye kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi. Sifa moja kubwa ya sentensi changamano ni kuwa na kishazi tegemezi ambacho hutegemea kishazi kingine huru ndani ya sentensi hiyo. Msingi muhimu wa uhusiano ndani ya sentensi hizo ni ule wa kishazi kimoja kutegemea kingine
Sentensi changamano ina muundo wenye vishazi virejeshi. Mfano: Gari liliopinduka jana jioni halikuharibika hatata kidogo.

Sentensi ambatano
Hii ni sentensi inayojengwa na sentensi mbili au zaidi zilizounganishwa kwa kutumia viunganishi kama vile likini, wala, au, na, nakadhalika.
Miundo ya sentensi ambatano
 • Miundo yenye sentensi sahili tu. Mfano: Mwalimu anafundisha wakati wanafunzi wanapiga kelele.
 • Miundo yenye sentensi sahili na changamano. Mfano: Walinzi waliposhindwa polisi waliwasaidia lakini hawakuweza kuwakamata majambazi.
 • Miundo yenye sentensi changamano tu. Mfano: Barabara zilizojengwa na wakoloni zimedumu hadi leo wakati zile zilizojengwa na Wachina hata mwezi hazifikishi.
 • Miundo yenye vishazi visivyounganishwa kwa viunganishi.
Uchanganuzi wa sentensi
Uchanganuzi wa sentensi ni mchakoto unaohusika na kuchanganua vipashio vyote vinavyuonda sentensi kuanzia ngazi ya kategoria ya neno. Katika kipengele hiki utaweza kujifunza hatua muhimu za kuzingatia wakati wa uchanganuzi wa sentensi. Pia utajifunza njia mbalimbali zinazotumika katika uchanganuzi wa sentensi.

Hatua za uchanganuzi wa sentensi
 • Kutaja aina ya sentensi, yaani kama ni sahili, changamano au ambatano.
 • Kutaja sehemu zake kuu, yaani kiima na kiarifu au kirai nomino na kirai kitenzi.
 • Kutaja sehemu kuu za kiima na kiarifu au sehemu kuu za kirai nomino na kirai kitenzi.
 • Kutaja sehemu zote za maneno yaliyomo katika sentensi hiyo.
Njia za uchanganuzi wa sentensi

Njia ya mishale/mistari
Mfano
Uchanganuzi wa sentensi kwa njia ya mishale


Njia ya visanduku/jedwali
Mfano
S.S
KN
KT
N
KH
T
KN
H
KN
N
KV
N
V
KE
E
Mtu
Mwenye
Ulemavu
anacheza
mpira
mzuri
sana
Njia ya matawi

Mfano
Uchaganuzi wa sentensi kwa njia ya matawi
Mifano mingine ya uchanganuzi wa sentensi ambatano; (Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti)

Njia ya jedwali
Mfano
Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti
S.A
S1
U
S2
KN
KT
KN
KT
N
KV
T
KE
W
T
V
E
Watu
wengi
walimwamini
Sana
Lakini
Yeye
aliwasaliti
Kwa njia ya matawi
Mfano
Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti
Kwa njia ya mishale
Mfano
Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti


                        MADA YA TATU: MAENDELEO YA KISWAHILI
Asili ya Kiswahili
Ushahidi wa Kimsamiati na Kimuundo unaothibitisha Ubantu wa Kiswahili
Neno asili ni jinsi kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza. Kutokana na fasili hii tunaona kwamba jambo au kitu kinaweza kutokea kibahati kama ilivyo katika lugha au linaweza kuanzishwa.
Hivyo basi asili ya lugha ya Kiswahili bado ni mjadala mrefu ambapo wataalamu mbalimbali wanahitilafiana juu ya asili au chimbuko la lugha ya kiswahili. Wapo wanaokinasibisha kiswahili na kiarabu kwa kutumia kigezo cha msamiati na dini ya kiislamu. Wengine wanashikilia msimamo kuwa kiswahili ni kibantu kwa kutumia hoja za kiisimu na kihistoria. Wapo wanaokinasibisha kiswahili na uchotara baadhi yao wanaoshikilia msimamo huu ni Freeman Grenville na Homo Sasson
Kuna nadharia mbalimbali zinazojaribu kuelezea asili ya Kiswahili, miongoni mwa hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:

Kiswahili ni Kiarabu
Hapa Kiswahili kimefasiliwa kuwa asili yake ni kiarabu, wanaoshikilia mtazamo huu wanahoji kwamba katika lugha ya Kiswahili kuna maneno mengi ya Kiarabu. Pia wanaeleza kuwa asili ya Kiswahili ni pwani na kwa kuwa wenyeji wa pwani ni Waislamu na kwa kuwa uislamu uliletwa na Waarabu basi hii lugha ya pwani nayo itakuwa imeletwa na Waarabu. Vigezo hivyo vyote vina udhaifu mkubwa kwa sababu havikukitwa katika misingi ya kitaalamu ya uainishaji lugha.

Kiswahili ni lugha Chotara
Mtazamo huu umezua ubishi mkubwa kwani hata baadhi ya wazawa wamejinasibisha na uarabu na ushirazi. Wanaofasili Kiswahili kama lugha chotara wanadai kuwa Kiswahili kimetokana na mchanganyiko wa lugha ya Kiarabu na lugha za Kibantu. Hivyo Waswahili ni watu waliotokana na wanaume wa Kiarabu na wanawake wa Kibantu.

Kiswahili ni lugha ya Vizalia
Waumini wa mtazamo huu wanadai kuwa Kiswahili kilianza kama pijini ya Kiarabu na baadae kukomaa na kuwa kreoli. Pijini ni lugha ambayo imetokana na mchanganyiko wa lugha mbili tofauti yaani Kiarabu na lugha za Kibantu. Na kreoli ni lugha inayozungumzwa na watoto waliozaliwa na baba Mwarabu na mama Mbantu.

Kiswahili ni Kikongo
Nadharia hii inafafanua kuwa lugha ya Kiswahili ilianzia huko Kongo na kusambaa katika pwani ya Afika Mashariki. Wabatu walipofika Afrika Mashariki waliingia kwa makundi na katika nyakati mbalibali. Makundi hayo yalianza kujigawa na kutawanyika, matokeo ya kugawanyika huko ni kutokea kwa makundi mbalimbali ya wabantu. Inasadikika kuwa baadhi ya Wabantu walifanya maskani yao ya kudumu katika mabonde ya kaskazini mwa mto tana. Kikundi hiki cha wabantu ndicho inasadikiwa kuwa chimbuko la Kiswahili

Kiswahili ni Kibantu
Mtazamo huu ni ule unaoamini kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu ambapo lugha za Kibantu zilikuwepo hata kabla ya majilio ya wageni kutoka Ajemi, Arabuni, India, China na kwingineko. Katika mtazamo huu lugha ya Kiswahili inaingizwa katika kundi la lugha za Kibantu. Ama kwa hakika mtazamo huu ulipata mashiko sana kuanzia karne ya ishirini, ulishadidiwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na weledi wa isimu, historia, akiolojia na ethnografia. Wanaisimu waliothibitisha kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu ni pamoja na Bleek (1862), Meinholf. C (1932), Malcom Guthrie (1967, 1970, 1971), Doke (1935, 1945) na wengineo. Vigezo vilivyotumika kufafanua kuwa Kiswahili ni kibantu ni pamoja na:
 • Msamiati
 • Mofolojia
 • Mfumo wa sauti
 • Mfumo wa toni
 • Mfumo wa ngeli
 • Mpangilio wa maneno
Ubantu wa Kiswahili: Kigezo cha Kiisimu
Kigezo hiki cha kiisimu kimetumiwa na wataalam mbalimbali katika kuonesha ubantu wa Kiswahili Massamba (1999) amewataja wataalam mbalimbali ambao wamehusika na utafiti juu ya ubantu wa Kiswahili, wataalam hao ni pamoja na Carl Meinhof katika kitabu chake chaIntroduction to the phonology of the Bantu language,Duke (1935 – 1945), Malcom Guthrie (1967), Dereck Nurse na Thomas Spear (1985). Hawa walijadili ubantu wa Kiswahili kwa kutumia kigezo cha kiisimu, kihistoria na kiakiolojia.
Katikakigezo cha kiisimu vipengele vinavyoangaliwa ni kama vile kufanana kwa msamiati wa msingi, muundo wa kifonolojia, muundo wa kimofolojia, muundo wa kisintaksia mpangilio wa ngeli za majina.
Mizizi ya msamiati wa msingiwa lugha za kibantu na Kiswahili hufanana kwa kiasi kikubwa, mifano ifuatayo huweza kuonesha ukweli huu.

Mfano
Kiswahili
Kikurya
Kinyiha
Kijita
Maji
Amanche
Aminzi
Amanji
Jicho
Iriso
Iryinso
Eliso
Katika mifano hiyo hapo juu tunaona kuwa mizizi maji, manche, minzi, manji inafanana kwa kiasi kikubwa, kwa hiyo huu ni ushahidi tosha kutuonesha kuwa kuna uhusiano wa kinasaba kati ya Kiswahili na lugha za kibantu.
Piamofolojia ya Kiswahili na lugha za kibantuhufanana kwa kiasi kikubwa, yaani mfumo wa maumbo ya maneno ya lugha ya Kiswahili na lugha za kibatu hufanana. Kwa mfano, namna viambishi vinavyopachikwa katika mzizi wa maneno hufuata kanuni ileile kama inavyotumika katika lugha ya Kiswahili yaani viambishi vinaweza kupachikwa kabla au baada ya mzizi na huwa na uamilifu bayana.

Mfano
Hebu tuchunguze mifano ifuatayo:
Kiswahili
Kisukuma
Kisimbiti
Kinyiha
A-na-lim-a
a-le-lem-a
a-ra-rem-a
i-nku-lim-a
a-na-chek-a
A-le-sek-a
a-ra-sek-a
a-ku-sek-a
Kwa kuangalia mifano hii utagundua kwamba katika kutenganisha viambishi hufuata kanuni moja kwamba mahali kinapokaa kiambishi kwa mfano cha njeo, ndipo pia hukaa kwa upande wa lugha za kibantu, kwa mfano –na- na –ra- katika lugha ya kisimbiti. Hivyo tunaweza kusema kuwa kuna unasaba baina ya lugha hizi
Vilevilesintaksiaya lugha ya Kiswahili na lugha za kibantu hufanana kwa karibu sana. Kwa mfano jinsi yampangilio wa vipashio na kuunda sentensihufanana yaani mpangilio wa maneno hufuata kanuni maalum ambazo hufanana katika Kiswahili na lugha za kibantu. Katika Kiswahili sentesi inakuwa na pande mbili yaani upande wa kiima na upande wa kiarifu, katika upande wa kiima kipashio chake kikuu ni nomino na katika upande wa kiarifu kipashio chake kikuu ni kitenzi. Hii inamaana kwamba katika kuunda sentensi ni lazima nomino ianze na baadaye kitenzi.

Mfano
Hebu tuangalie mifano ifuatayo:
Kiswahili
Mama / anakulaN (K) T (A)
Kijita
Mai / kalyaN(K) T (A)
Kihehe
Mama/ ilyaN(K) T(A)
Kihaya
Mama / nalyaN(K) T(A)
Katika mifano hii tumeona kwamba muunndo wa kiima-kiarifu katika lugha za kibantu unafanana sana na ule wa Kiswahili yaani nomino hukaa upande wa kiima halikadhalika kitenzi hukaa upande wa kiarifu, kwa hiyo kwa mifano hii tunaweza kusema kuwa lugha ya Kiswahili ni jamii ya lugha za kibantu.
Piamfumo wa sauti (fonolojia)wa lugha za kibantu unafana sana na ule wa Kiswahili, yaani mpangilio wa sauti katika kuunda silabi, na miundo ya silabi kwa ujumla hufanana. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili hakuna muundo wa silabi funge yaani silabi ambayo inaishia na konsonanti, muundo asilia wa silabi za Kiswahili ni ule unaoishia na irabu vilevile katika lugha za kibantu hufuata muundo wa silabi wazi, yaani silabi zote huishia na irabu.

Mfano
Mifano ifuatayo hufafanua zaidi:
Kisawhili
Baba
K+I+K+I
Kikurya
Tata
K+I+K+I
Kiha
Data
K+I+K+I
Kijita
Rata
K+I+K+I
Kipare
Vava
K+I+K+I
Tanbihi: K= konsonanti I= irabu.
Kwa mifano hii tunaona kwamba mifumo ya sauti katika lugha za kibantu hufanana na ule wa Kiswahili, kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa lugha hizi ni za familia moja.
Pia vilevilemfumo wa ngeli za majinakatika lugha ya Kiswahili hufanana sana na ule wa kibantu hususani katika upachikaji wa maumbo ya umoja na wingi na maumbo ya upatanisho wa kisarufi. Katika lugha ya Kiswahili viambishi vya umoja na wingi hupachikwa mwanzoni kabla ya mzizi wa neno, hivyohivyo katika lugha za kibantu


Kwa mfano:
Umoja
 Wingi
Kiswahili
m-tu
wa-tu
Kikurya
mo-nto
abha-nto
Kiha
umu-ntu
abha-ntu
Kikwaya
mu-nu
abha-nu
Mifano hiyo hapo juu inadhihirisha wazi kwamba vipashio vyote vya umoja na wingi hujitokeza kabla ya mzizi wa neno, hivyo ni dhahiri lugha hizi zina uhusiano wa nasaba moja.
Vilevile katikaupatanisho wa kisarufilugha za kibantu na Kiswahili huelekea kufanana viambishi vya upatanisho wa kisarufi hususani viambishi vya nafsi.

Mfano wa viambishi vya nafsi
Kiswahili
Mtotoa-nalia
Kizanaki
Umwanaa-rarira
Kisukuma
Ng’wanaa-lelela
Kikurya
Omonaa-rakura
Tunaona hapo juu kwamba kiambishi ‘a’ cha upatanisho wa kisarufi hujitokeza katika lugha zote, hivyo tunashawishika kusema kuwa Kiswahili kina uhusiano mkubwa na kibantu.
Pamoja na ushahidi wa kiisimu kutupatia vithibitisho tosha juu ya ubantu wa Kiswahili pia kuna ushahidi mwingine kama vile ushahidi wa kihistoria, kiakiolojia na kiethinolojia.

Ushahidi wa Kihistoria
Ushahidi wa kihistoria huchunguza masimulizi na vitabu mbalimbali vya kale ambavyo huelezea asili na chimbuko la wakazi wa upwa wa Afrika Mashariki. Vilevile ugunduzi wa kiakiolojia huonesha kuwa kulikuwa na wakazi wa asili wa upwa wa Afrika Mashariki ambao walikuwa na utamaduni wao na maendeleo yao hata kabla ya kuja kwa wageni. Katika ushahidi wa kiethinolojia, huchunguzwa tarihi mbalimbali zinazojaribu kutoa historia ya watu wa pwani ya Afrika Mashariki na lugha yao.
Kwa ujumla vyanzo hivi vyote huonesha kuwa pwani ya Afrika mashariki ilikuwa na wakazi wake wa asili ambao walikuwa na lugha yao, utamaduni wao na pia maendeleo yao, vyanzo hivi pia huhitimisha kwa kusema kuwa lugha ya wakazi hawa ilikuwa ni Kiswahili.
Jinsi Miundo ya Kiswahili inavyofanana na Miundo ya Lugha nyingine za Kibantu
Fafanua jinsi miundo ya Kiswahili inavyofanana na miundo ya lugha nyingine za Kibantu
Miundo ya lugha ya za kibantu inafanana na lugha ya Kiswahili na kufanana huko hutokea katika miundo silabi ambapo zote huishia na irabu na siyo konsonanti, miundo ya sentensi, miundo ya vitenzi vya Kiswahili ni sawa na ile ya Kibantu. Kwa mfano vitenzi vya Kiswahili na kibantu vina uhusiano mkubwa hasa katika viambishi, mnyumbaliko na pamoja na mianzo na miisho ya vitenzi. Mada hii imefafanuliwa vizuri katika mada iliyotangulia hapo juu.

Kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania katika enzi ya Waarabu
Katika karne ya kumi na tisa Afrika Mashariki iliingia kwenye mahusiano na mataifa mengine kama vile Marekani, Ujerumani na Uingereza. Mahusiano haya ni baada ya watu wa pwani kuwa na uhusiano wa muda mrefu wa kibiashara na Waaarabu, hawa waliweka athari kubwa katika kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili. Wageni kutoka Ulaya walipoingia Afrika Mashariki walifanya biashara, shughuli za kidini (mishenari), elimu na utawala. Kama ilivyokuwa katika kipindi cha Waarabu, uwepo wao pia ulikuwa na athari katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki na kwingineko.

Ukuaji wa Kiswahili Kimsamiati nchini Tanzania katika Enzi ya Waarabu
Waarabu hasa katika pwani ya Afrika Mashariki walifanya biashara ikiwemo biashara ya watumwa. Ilikuwepo misafara mbalimbali ya biashara kutoka pwani hadi bara. Katika misafara hiyo Kiswahili ndio ilikuwa lugha ya mawasiliano hivyo Kiswahili kikaenea pia katika sehemu za bara.
Kuna mambo kadhaa waliyofanya waarabu ambayo yalichangia kukua kwa lugha ya Kiswahili. Waarabu walichangia kukua kwa lugha ya Kiswahili kama ifuatavyo:

Biashara
Waarabu walifanya biashara kati ya pwani na sehemu za bara, katika biashara yao walichangia kwa kiasi kikubwa uenezaji wa lugha ya Kiswahili. Lugha kuu ya mawasiliano na ya kibiashara iliyotumiwa na wafanya biashara wa kiarabu ilikuwa ni Kiswahili, kwa hiyo kwa njia hii waliweza kueneza Kiswahili kuanzia pwani hadi maeneo ya bara kama vile Tabora, Kigoma hadi mashariki mwa Kongo.

Dini
Dini pia ni jambo ambalo liliweza kuchangia ueneaji wa lugha ya Kiswahili enzi za waarabu. Waarabu walipokuja walitaka kueneza dini yao kwa undani kabisa. Kwa hivyo iliwabidi kuanzisha madarasa ambayo walitumia kufundishia, lugha iliyokuwa ikitumiwa ni lugha ya Kiswahili. Na hivyo hii ikasaidia kuenea kwa lugha ya Kiswahili.

Maandishi ya kiarabu
Waarabu pia walileta hati zao zilizotumiwa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo kupitia hati za kiarabu maandishi mbalimbali ya lugha ya Kiswahili yaliweza kuhifadhiwa, hivyo Kiswahili kiliweza kukua kwa vile kingeweza kuhifadhiwa katika maandishi na kusomwa wakati wowote.

Kuoana
Pia vilevile Waarabu waliofika pwani waliweza kuoana na wabantu, hii ilisababisha kizazi kipya kutokea. Na kwa sababu hiyo watoto walichukua maneno mengi kutoka kwa baba na mama yao na hivyo kuongeza msamiati katika lugha Kiswahili.

Ueneaji wa Kiswahili nchini Tanzania katika Enzi ya Waarabu
Waarabu walieneza Kiswahili nchini Tanzania kupitia biashara, kuoana na wabantu au wenyeji wa pwani, kupitia dini na maandishi ya hati za kiarabu ambayo yalitumika kuhifadhi maandishi mbalimbali ya lugha ya Kiswahili.

Kukua na kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania katika enzi ya Wajerumani
Wajerumani waliingia katika pwani ya Afrika Mashariki katika miaka ya 1875, walifanya kila jitihada kuwatawala Waafrika ambapo katika utawala wao walifanya biashara, waliendesha shughuli za kiutawala, za kidini na kielimu. Katika shuguli zote hizo Kiswahili ndio ilikuwa lugha ya mawasilino hivyo kukikuza na kukiendeleza Kiswahili
Walipongia katika pwani ya Afrika Mashariki walikuta Kiswahili kimekwisha enea kwa kiasi kikubwa. Kuna mambo waliyoyafanya ambayo yalisaidia kukua na kuenea kwa Kiswahili kama ifuatavyo:

Kutoa mafunzo ya lazima ya lugha ya Kiswahili kwa wafanyakazi wa serikali
Waliwalazimisha wafaanyikazi wote wa serikali kujifunza kiswashili, kwa sababu sheria ilikuwa ni kwamba pasipojua Kiswahili huwezijiriwa katika serekali ya mjerumani. Kwa hiyo saula hili lilisababisha watu kujifunza lugha ya Kiswahili ili waweze kuajiriwa. Wafanyakazi ambao ilikuwa ni lazima wajifuze Kiswahili ni pamona na maakida.
Wajerumani wenyewe walilazimika kujifunza kiswahili ili waweze kuwasiliana na wenyeji kwa urahisi na hivyo kurahisisha shuguli zao za kiutawala.

Ujenzi wa shule
Shule zilifunguliwa kufundisha watu weusi ili waje wawe wasidizi wao katika utawala wa wajerumani, na lugha iliyokuwa ikitumika kufundisha masomo ilikuwa ni lugha ya Kiswahili
Kuenea kwa utawala wa Wajerumani nchi nzima
Utawala wa wajerumani ulikuwa kwenye kila kona ya nchi. Na kwa kuwa wafanya kazi wa serikali ya wakati huo ilikuwa ni lazima wafahamu Kiswahili, kwa hiyo kila sehemu palipokuwa na ofisi za serikali nchi nzima kulizungumzwa Kiswahili.

Shughuli za kiuchumi
Pia katika shuguli za mashamba, wajerumani walichukua vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi, na kwa kuwa kila mmoja alikuwa na lugha yake tofauti, kwa hiyo lugha pekee iliyowaunganisha katika mawasiliano kwenye eneo la kazi ilikuwa ni Kiswahili.
Kwa hiyo kutokana na sababu kwamba utawala wa kijerumani ulitoa msukumo mkubwa katika matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye shughuli zao za kiutawala, hivyo suala la ueneaji wa Kiswahili lisingeepukika.

Ueneaji wa Kiswahili nchini Tanzania katika Enzi za Wajerumani
Wajerumani walichangia kwa sehemu kubwa kuenea kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania enzi za utawala wao. Mambo yaliyochangia kuenea kwa lugha ya Kiswahili enzi za utawala wa Wajerumani ni pamoja na dini, elimu, shughuli za utawala na shughuli za kiuchumi kama vile kilimo.               MADA YA NNE: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.

Maana ya Uhakiki
Dhana ya Uhakiki
Uhakiki ni kitendo cha kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Hii ina maana kwamba uhakiki wa kazi za fasihi hautoki katika ombwe, kuna kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza kufanya uhakiki, na hii ndio sababu kuna nadharia kadha wa kadha za uhakiki wa kazi za kifaishi. AU kwa lugha rahisi tunaweza kusema, uhakiki ni uchambuzi wa kina wa kazi za fasihi kama vile riwaya, tamthiliya na mashairi kwa lengo la kufafanua vipengele vya fani na maudhui.

Misingi ya Uhakiki
Kwa ujumla mhakiki wa kazi za fasihi anapofanya uhakiki wa kazi za kifasihi, huwa analenga vipengele viwili. Pengine analenga kuhakikifaniya kazi husika aumaudhuiya kazi hiyo na wakati mwingine vyote viwili. Kwa hiyo kupitia vipengele hivi ndipo atachambua vitu vingi kama vile ujumbe, falsafa, matumizi ya lugha, dhamira, mandhari na kadhalika.

Kuhakiki Fani
Katika utunzi wa kazi za kifasihi, Fani hutumika kama nyezo ya kuwasilisha mawazo ya mwandishi kwa njia ya kisanaa zaidi. Fani ni mbinu anayoitumia mwandshi ili kufikisha ujumbe kwa watu aliowakusudia.
Vipengele vya fani ni pamoja nawahusika, mandhari, lugha, muundo na mtindo.

Mtindo
Mtindo ni mbinu ya kipekee kifani na kimaudhui, zinazotofautisha msanii mmoja na mwingine. Kwa mfano, namna msanii anavyotumia lugha, anavyoteua msamiati, namna anavyosimulia hadithi yake (anaweza kutumia nafsi ya kwanza, ya pili au ya tatu). Kwa mfano katika riwaya ya “Barua Ndefu kama hii” iliyoandikwa na Mariama Ba ametumia mtindo wa barua ya kirafiki kuanzia mwanzo hadi mwisho, hii pia inaonesha mtindo wake wa kipekee.

Muundo
Muundo ni mpangilio wa kiufundi anaoutumia mwandishi katika kupangilia kazi yake. mpangilio na mtiririko wa kazi ya fasihi, kwa upande wa visa na mtukio.
Kuna aina mbili za kupangilia matukio
 1. Msago; hii ni namana ya moja kwa moja ya kusimulia matukio, yaani kuanzia tukio la kwanza hadi la mwisho kwa namna yalivyotukia. Huu ni muundo wa moja kwa moja.
 2. Urejeshi; huu ni usimuliaji wa kurukaruka hatua, yaani msimuliaji anaweza kuanzia katikati, akaja mwisho na kumalizia na mwanzo


Wahusika
Wahusika; ni watu au viumbe ambavyo mwandishi wa fasihi huwatumia ili kufanikisha ujumbe kwa jamii husika. Katika kazi ya fasihi mwandishi huwagawa wahusika katika makundi mawili yaani wahusika wakuu na wahusika wadogo.
Wahusika wakuu ni wale ambao wanajitokeza kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa kazi ya fasihi. Wahusika wadogo ni wale wote ambao wanajitokeza sehemu mbalimbali katika kazi ya fasihi kwa mfano, mwanzoni mwa kitabu hadi mwishoni mwa kitabu.
Wahusika hawa wawe ni wakuu au wadogo wanaweza kugawanyika katika makundi yafuatayo:
 1. Mhusika mviringo ni mhusika ambaye anabadilika kitabia na kimawazo kulingana na hali halisi ya maisha. Kwa mfano wanaweza kuanza kama watu wema lakini hali ya maisha ikawabadilisha na kuwa watu wabaya au wanaweza kuanza kama watu wabaya na hali ya maisha ikawabadilisha na kuwa watu wema.
 2. Mhusika bapa ni mhusika ambaye habadiliki kulingana na hali halisi ya maisha. Mfano; kama ni mwema basi atakuwa mwema kuanzia mwanzo wa hadithi hadi mwisho na kama ni mbaya basi atakuwa mbaya kuanzia mwanzo wa hadithi hadi mwisho.
 3. Mhusika shinda yuko katikikati ya mhusika papa na mviringo. Huongozwa na matendo ya hao wahusika wawili. Hajitokezi na msimamo wake imara.
Mandhari
Mandhari; hii ni sehemu ambayo matukio ya hadithi au masimulizi hutokea. Mandhari huweza kuwa halisi kama vile baharini, njiani, msituni, kijijini, mijini au ya kufikirika kama vile kuzimu, mbinguni, peponi n.k.

Lugha
Lugha ndio nyenzo kubwa ya msanii katika kazi za fasihi, miongoni mwa vipengele vya lugha ni tamathali za semi pamoja na semi.
Fani za Lugha
 • Tanakali za Sauti: Ni mbinu ya kutumia maneno yanayoiga sauti au hali fulani au namna kitendo kilivyofanyika.
 • Tashbiha: Hii ni mbinu ya lugha inayolinganisha vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno ya kulinganisha; ‘kama’, ‘mithili ya’, ‘sawa na’, ‘ja’. mfano, Mwembamba kama sindano.
 • Tashihisi: Hii ni mbinu ya kupatia kitu kisicho hai sifa za kiumbe mwenye uhai (sifa za kibinadamu). Mfano, "Sungura aliposhindwa, akasema sizitaki hizi mbichi".
 • Takriri: Ni mbinu ya kurudiarudia neno moja au kifungu cha maneno ili kusisitiza ujumbe fulani. Mfano, alikimbia, alikimbia, alikimbia hadi akashika nafasi ya kwanza.
 • Ukinzani: Ukinzani ni mbinu ya kusisitiza ujumbe kwa kuambatanisha maneno ya kinyume au yanayokinzana.
 • Sitiari: Ni mbinu ya kulinganisha vitu viwili moja kwa moja kwa kutumia kiungo ‘ni’ ama ‘kuwa’. Mfano; Maisha ni mlima, juma ni mwamba.
 • Taswira: Ni matumizi ya lugha/maneno yanayojenga picha ya hali au jambo fulani kwa msomaji.
 • Taashira: Ni matumizi ya lugha ya ishara kuwakilisha ujumbe fulani. Jina au kitu fulani kinatumika kumaanisha kitu kingine chenye uhusiano na kile kilichotumiwa.
 • Jazanda: Ni kulinganisha vitu viwili moja kwa moja bila kutumia viunganishi.
 • Majazi: Majazi ni pale tabia za wahusika zinapoambatana na majina yao halisi.
 • Lakabu: Ni mbinu ya mhusika kupewa/kubandikwa jina na wahusika wengine ama yeye mwenyewe kujibandika jina linalooana na tabia/sifa zake.
 • Chuku: Ni kutumia maneno yaliyotiliwa chumvi ili kusisitiza ujumbe fulani au kusifia kitu, kutilia Chumvi.
Semi
Ni fungu la maneno linapotumika kutoa maana nyingine, badala ya ile ya maneno yaliyotumika. Semi hutumika kuficha ukali wa maneno au kupamba lugha. Kuna aina mbili za semi:
 • Nahau – ni usemi unaotumia maneno ya kawaida kwa lengo la kufikisha maana iliyotofauti na maana ya kawaida ya maneno hayo. Nahau huwa na vitenzi.
 • Misemo – ni semi fupifupi ambazo hutumiwa mara kwa mara kwa lengo la kuleta maana maalumu. Misemo haina vitenzi.
 • Maswali ya Balagha: Tashititi au maswali ya balagha ni maswali yanayoulizwa na msimulizi au mhusika ambayo hayahitaji jibu.
 • Uzungumzi Nafsiya: Mhusika hujizungumzia, ama kwa kuongea au kuwaza, bila kukusudia kusikika na yeyote.
 • Ritifaa: Mbinu ya kuzungumza na mtu aliyekufa (au asiyekuwepo) kana kwamba yuko pamoja nawe.
 • Kuchanganya Ndimi: Kuweka maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili. Mfano, "alisimama kwanza kwa muda, before he went aliniambia nisimwambie mtu yeyote yule, you know!"
 • Kuhamisha Ndimi: Ni kuingiza sentensi ya lugha nyingine katika kifungu cha lugha ya Kiswahili. Kinyume na Kuchanganya ndimi (ambapo mwandishi huchanganya maneno katika sentensi moja, katika kuhamisha ndimi, sentensi kamilifu ya lugha nyingine hutumika miongoni mwa sentensi za Kiswahili sanifu. Mfano: Kazi hii ni ngumu sana, sitaweza kuifanya. People are trying to convince me to stay here but I think I can't, I must go!
 • Mathali: Methali ni misemo ya hekima yenye maana iliyofumbwa. Mhusika, mwandishi wa fasihi anaweza kutumia methali kupitisha ujumbe.
Mbinu nyingine za Kisanaa
 • Kinaya: Kinaya ni mambo katika sanaa kuwa kinyume na matarajio ya hadhira.
 • Kejeli; Kejeli ni mbinu ya sanaa inayotumia maneno kudharau au kukemea kitendo au mtu fulani.
 • Taharuki; Taharuki ni mbinu ya kusimulia au kuandika riwaya/hadithi kwa kufanya hadhira na/au wahusika wajawe na hamu ya kutaka kujua kitakachotokea baadaye; hamu ya kutaka kuendelea kusoma/kusikiliza. Baadhi ya hadithi huishia kwa taharuki na kuilazimisha hadhira yake ijikamilishie au ibaki ikijiuliza maswali.
 • Sadfa; Sadfa ni kugongana kwa vitendo viwili vinavyohusiana kana kwamba vilikuwa vimepangwa, japo havikuwa vimepangiwa.
 • Kisengere Nyuma; Mwandishi ‘hurudi nyuma’ na kuanza kusimulia kisa kilichokuwa kimetendeka kabla ya alichokuwa akisimulia. Aidha, mwandishi hubadilisha wakati wa masimulizi na kuwa wakati wa kisa hicho. Hutumika sana kuonyesha mhusika anapokumbuka kitu, au kutupatia msingi wa jinsi mambo yalivyoanza.
 • Kisengere Mbele; Mwandishi anapobadilisha wakati na kusimulia mambo yatakavyokuwa siku za usoni; au kutumia lugha isiyo moja kwa moja kutabiri yatakayojiri. Utabiri.
Kuhakiki Maudhui
Maudhui; Maudhui katika kazi ya fasihi ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma msanii hadi akatunga na kusanii kazi fulani ya kifasihi. Vipengele vya maudhui ni pamoja na dhamira, migogoro, falsafa ujumbe na msimamo.
 1. Dhamira; hili ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Dhamira ni sehemu tu ya maudhui na aghalabu dhamira kuu ndio hujenga kiini cha kazi ya fasihi. Dhamira zimegawanyika katika makundi mawili, kuna dhamira kuu na dhamira ndogondogo.
 2. Migogoro; hii ni mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi za fasihi. Migogoro inaweza kuwa kati ya wahusika, familia zao, matabaka yao, au hata katika nyadhifa mbalimbali. Vilevile migogoro yaweza kuwa ya kiuchumi, kijamii, mogogoro ya nafsi, na migogoro ya kisiasa ambayo hujitokeza katika mitazamo tofauti kulingana na mtiririko wa visa na matukio yanavyopangwa na mwandishi.
 3. Ujumbe; mwandishi anapoandika kazi yake huwa na ujumbe ambao hutaka uifikie jamii aliyoikusudia. Ujumbe katika kazi fasihi ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi ya fasihi. Katika kazi ya fasihi dhamira kuu hubeba ujumbe wa msingi na dhamira ndogondogo hubeba ujumbe ambao husaidia kuujenga au kuupa uzito zaidi ujumbe wa msingi.
 4. Msimamo; katika kazi ya fasihi, mawazo, mafunzo na falsafa ya msanii hubainisha msimamo wake kuhusu masuala mbalimbali ya kijamii. Msimamo ni ile hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili huweza kukataliwa na wengi lakini akalishikilia tu. Msimamo ndio huweza kuwatofautisha wasanii wawili au zaidi wanaoandika kuhusu mazingira yanayofanana. Kwa mfano, katika tamthilia ya “Pesa zako zinanuka” mwandishi anamsimamo wa kimapinduzi kwani amejadili matatizo yanayochangia kukwama kwa ujenzi wa jamii mpya.
 5. Falsafa ni mawazo ya busara yenye kutawaliwa na misingi mahususi juu ya asili na maana ya ulimwengu na maisha ya mwanadamu. Ni msimamo wa msanii katika maisha juu ya utatuzi wa matatizo katika jamii. Falsafa ya mwandishi inaweza kujulikana kwa kusoma kazi zake zaidi ya moja.
 6. Mtazamo ni hisia au uelewa wa mwandishi juu ya jambo fulani. Kwa mfano anaweza kutazama jambo fulani kwa mtazamo wa kidini, au anaweza kutazama jambo fulani kwa mtazamo wa kisiasa au kisayansi.
 7. Mafunzo; ni mawazo ya kuelimisha yanayopatikana katika dhamira mbalimbali za kazi ya fasihi.

Kufaulu na Kutofaulu kwa mwandishi
Kufaulu au kutofaulu kwa mwandishi kunategemea jinsi alivyoweka uwiano mzuri kati ya fani na maudhui kwa namna ambavyo inaleta uhalisia. Mfano, endapo msanii atakuwa na mhusika Mkongo lakini akawa anazungumza kiswahili kilichojaa misemo na nahau alafu kimenyooka kama mtu wa pwani itakuwa vigumu kusema amefaulu kwani hakuna uwiano mzuri kati ya mhusika mwenyewe na lugha anayoitumia. Kiswahili cha Kongo ni tofauti kabisa na kiswahili kinachozungumzwa na watu wa pwani (Tanzania).

Uhakiki wa Fani katika Kazi za Fasihi Andishi

Uhakiki wa Fani katika Tamthiliya

Uhakiki wa fani katika Ushairi

Uhakiki wa Maudhui katika Kazi za Fasihi Andishi

Uhakiki wa Maudhui katika Tamthiliya

Uhakiki wa Maudhui katika Ushairi


               MADA YA TANO: UTUNGAJI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI
Top of Form
Bottom of Form
Utungaji wa Hadithi
Mikondo ya Hadithi
Kazi za fasihi andishi ni sanaa, yaani zinahitaji ubunifu wa mwandishi ili ziwe katika mwonekanao huo wa kisanaa. Fasihi andishi hutumia lugha na wala sio lugha tu bali lugha ya kisanaa, kama tulivyokwishaona katika mada zilizotangulia kwamba lugha ni kipengele muhimu sana katika fasihi. Ili kazi ya kifasihi ya msanii husika iwe nzuri na ya kuvutia, masanii hana budi kuwa na ubunifu wa hali ya juu katika kutumia lugha.
Msanii awe na uwezo wa kupangilia maneno, kuteua maneno katika hali ya ujumi lakini pia yakiwa yamebeba ujumbe unaoigusa hadhira yake. Kwa maana hii mwandshi wa kazi za kifasihi, iwe riwaya au tamthilia ni lazima azingatie sana lugha, kwani lugha ndio nyenzo kuu ya usanaa wa fasihi kwa ujumla.
Kuna hatua kadhaa za kuzingatia wakati wa kuandika kazi ya kisanaa, hatua hizo ni kama zifuatazo:
 • Kuwa na kisa/wazo unalotaka kuliandikia: Katika jamii kuna mambo mengi sana yanayotendeka, msanii anaweza kupata wazo la kiubunifu kutokana na mambo hayo yanayotendeka katika jamii. Kama tujuavyo fasihi andishi kazi yake ni kuonesha yale yanayotendeka katika jamii, kwa hiyo msanii anaweza kutumia fursa hiyo ili kuweka wazi mambo yanayoendelea katika jamii. Kwa mfano mwandishi naweza kutunga kazi ya kibunifu kuhusu, ufisadi, umasikini, mapenzi, ndoa, maisha yake mwenyewe, ushirikina, jambo lolote analoliamini katika maisha (falsafa yake). Kwa hiyo hatua ya kwanza kwa msanii kabala ya kuandika ni kuelewa vizuri jambo analotaka kuandikia. Pia katika hatua hii msanii anaweza kubuni jina la hadithi yake, pia hii inaweza kumsaidia katika upangaji wa visa na matukio ya hadithi yake.
 • Kuchagua umbo la kazi ya fasihi: Msanii akishapata wazo la kuandika, sasa inambidi achague jinsi atakavyoliwasilisha wazo lake hilo. Yaani anaweza kuchagua endapo aandike hadithi fupi, riwaya au tamthiliya, au ushairi au utenzi. Sasa uchaguzi wa umbo la kazi ya fasihi unategemeana na uwezo wa msanii katika tanzu hizo, kuna mwingine anapenda tamthiliya lakini kuandika riwaya hawezi, kuna mwingine anaona kuandika ushairi ni rahisi na kuna mwingine hawezi. Kwa hiyo ubunifu wa msanii utadhihirika katika utanzu ule anaoumudu vizuri zaidi.
 • Kubaini hadhira: Mwandishi kujua yule anayemwandikia ni suala la msingi sana. Hadhira ipo ya watu wa aina mbalimbali, watoto, watu wazima, wasomi, wenye elimu ndogo, wakulima, wanasiasa n.k. Sasa mwandishi akishabaini hadhira anayoindikia itamsaidia kuteua lugha ya kuandikia, kwa mfano kama ni watoto, hatutegemei mwandishi kutumia lugha ngumu, misemo na nahau nyingi.
 • Kubuni wahusika na mandhari: Mwandshi baada ya kujua kazi yake inahusu nini sasa inambidi abuni wahusika wa hadithi yake. Wahusika wanaweza kuwa ni watu, wanyama, mimea, mazimwi, malaika n.k. Pia ni lazima abaini mazingira ambamo visa vyote vya hadithi na matukio yatakapofanyika. Mandhari yanaweza kuwa baharini, kijijini, mjini, mbinguni, kuzimu n.k
 • Kupanga msuko wa visa na matukio: Msuko wa visa na matukio ni muhimu sana katika usimulizi wa hadithi. Sasa kama mwandishi amaeamua kuwasilisha kazi yake kwa njia ama ya hadithi fupi au riwaya au tamthiliya ni vema ajue namna visa na matukio vitakavyopangwa. Katika kufanya hivi maswali yafuatayo ni muongozo mzuri katika kupangilia ploti: Hadithi yangu itaanzaje? Mgogoro utaanzaje? Ni kati ya nani na nani? Je, kilele cha mgogoro ni nini? Je, ni mhusika mkuu kubakwa na kuambukizwa VVU? Hadithi yangu inaishaje? Je mhusika mkuu ashindwe? Atorokee nje ya nchi? Afungwe? Abadilike Au maadui ndio wafungwe au wafe? Au wabadilike?
 • Kuanza kuandika: Sasa baada ya kupitia hatua hizo zote, mwandishi sasa anaweza kuanza kuandika. Mchakato wa kuandika hua ni mrefu na mwandishi anaweza kujikuta anafuta mara nyingi kile alichokiandika, hii ni kutokana na kwamba mambo mengi ya kuandika huwa yanakuja wakati mwandishi ameanza kuandika kazi husika. Hata hvyo sio vibaya kufanya hivi, hii pia inasaidi kuwa na zao bora la fasihi.
Utungaji wa hadithi
Hadithi ni masimulizi ya kubuni yaliyoandikwa kinathari inaweza kuwa na wahusika wengi, matukio mengi na mandhari mapana (inategemena na aina ya hadithi, iwapo ni hadithi fupi wahusika wake huwa ni wachache na pia matukio ni machache, mandhari yake pia ni finyu). Kuna aina zifuatazo za hadithi kulingana na kigezo cha urefu au maudhui. Kwa kigezo cha urefu kuna Hadithi Fupi na Riwaya. Kutokana na maudhui kuna Riwaya Dhati na Riwaya Pendwa.
Riwaya dhati ni zile zinazozungumzia masuala muhimu ya kijamii, kama vile uonevu wa tabaka la chini, rushwa, uongozi mbovu n.k
Riwaya pendwa ni hadithi zenye lengo la kuburudisha, kutokana na usimuliaji wake uliojaa taharuki na fantasia. Mambo yanayosimuliwa katika riwaya hizi ni yale yanayogusa hisia za watu kwa urahisi kama vile mapenzi, mauaji, ujasusi n.k.

Mikondo ya uandishi wa hadithi
Mkondo wa hadithi ni mwelekeo ambao mwandishi anaufuata katika utunzi wa kazi yake. Mikondo ya utunzi wa hadithi ni pamoja na hii ifuatayo:
 1. Mkondo wa kiwasifu; mkondo huu huhusisha hadithi zote zinazosimulia maisha ya watu. Ni riwaya ambayo inasimulia maisha ya mtu toka alipozaliwa hadi wakati huo.
 2. Mkondo wa kitawasifu; hadithi zinazofuata mkundo huu ni zile zinazosimulia maisha ya mtu binafsi yaani mwandishi mwenyewe. Kwa mfano riwaya ya “maisha yangu baada ya Miaka hamsini”. (S.Robert)
 3. Mkondo wa kihistoria; hadithi katika mkondo huu zinahusu matukio ya kweli ya kihistoria yaliyotokea. Kwa mfano riwaya ya “Uhuru wa Watumwa”
 4. Mkondo wa kipelelezi; hizi ni hadithi zinazozungumzia upelelezi wa uhalifu fulani kama vile ujambazi, wizi, rushwa, mauaji n.k.
 5. Mkondo wa kimapenzi; katika mkondo huu zinaingia riwaya zote zinazozungumzia masuala ya mapenzi.
Utungaji wa hadithi fupi
Kama tulivyokwisha ona hapo nyuma sifa za hadithi fupi, basi katika utungaji wake mambo yafuatayo ni sharti yazingatiwe:
 1. Hadithi fupi inakuwa na mhusika mkuu mmoja ambaye anajitokeza sana kuliko wahusika wengine.
 2. Idadi ya wahusika ni ndogo ukilinganisha na wahusika wa kwenye riwaya.
 3. Mandhari ya hadithi fupi si mapana kama ilivyo katika riwaya
 4. Hadithi fupi inakuwa inaongelea dhamira kuu moja tu ambayo inaonekana toka mwanzo hadi mwisho wa hadithi.
Top of Form
Bottom of Form
Utungaji Wa Kazi Za Fasihi Andishi
Utungaji wa Hadithi
Mikondo ya Hadithi
Kazi za fasihi andishi ni sanaa, yaani zinahitaji ubunifu wa mwandishi ili ziwe katika mwonekanao huo wa kisanaa. Fasihi andishi hutumia lugha na wala sio lugha tu bali lugha ya kisanaa, kama tulivyokwishaona katika mada zilizotangulia kwamba lugha ni kipengele muhimu sana katika fasihi. Ili kazi ya kifasihi ya msanii husika iwe nzuri na ya kuvutia, masanii hana budi kuwa na ubunifu wa hali ya juu katika kutumia lugha.
Msanii awe na uwezo wa kupangilia maneno, kuteua maneno katika hali ya ujumi lakini pia yakiwa yamebeba ujumbe unaoigusa hadhira yake. Kwa maana hii mwandshi wa kazi za kifasihi, iwe riwaya au tamthilia ni lazima azingatie sana lugha, kwani lugha ndio nyenzo kuu ya usanaa wa fasihi kwa ujumla.
Kuna hatua kadhaa za kuzingatia wakati wa kuandika kazi ya kisanaa, hatua hizo ni kama zifuatazo:
 • Kuwa na kisa/wazo unalotaka kuliandikia: Katika jamii kuna mambo mengi sana yanayotendeka, msanii anaweza kupata wazo la kiubunifu kutokana na mambo hayo yanayotendeka katika jamii. Kama tujuavyo fasihi andishi kazi yake ni kuonesha yale yanayotendeka katika jamii, kwa hiyo msanii anaweza kutumia fursa hiyo ili kuweka wazi mambo yanayoendelea katika jamii. Kwa mfano mwandishi naweza kutunga kazi ya kibunifu kuhusu, ufisadi, umasikini, mapenzi, ndoa, maisha yake mwenyewe, ushirikina, jambo lolote analoliamini katika maisha (falsafa yake). Kwa hiyo hatua ya kwanza kwa msanii kabala ya kuandika ni kuelewa vizuri jambo analotaka kuandikia. Pia katika hatua hii msanii anaweza kubuni jina la hadithi yake, pia hii inaweza kumsaidia katika upangaji wa visa na matukio ya hadithi yake.
 • Kuchagua umbo la kazi ya fasihi: Msanii akishapata wazo la kuandika, sasa inambidi achague jinsi atakavyoliwasilisha wazo lake hilo. Yaani anaweza kuchagua endapo aandike hadithi fupi, riwaya au tamthiliya, au ushairi au utenzi. Sasa uchaguzi wa umbo la kazi ya fasihi unategemeana na uwezo wa msanii katika tanzu hizo, kuna mwingine anapenda tamthiliya lakini kuandika riwaya hawezi, kuna mwingine anaona kuandika ushairi ni rahisi na kuna mwingine hawezi. Kwa hiyo ubunifu wa msanii utadhihirika katika utanzu ule anaoumudu vizuri zaidi.
 • Kubaini hadhira: Mwandishi kujua yule anayemwandikia ni suala la msingi sana. Hadhira ipo ya watu wa aina mbalimbali, watoto, watu wazima, wasomi, wenye elimu ndogo, wakulima, wanasiasa n.k. Sasa mwandishi akishabaini hadhira anayoindikia itamsaidia kuteua lugha ya kuandikia, kwa mfano kama ni watoto, hatutegemei mwandishi kutumia lugha ngumu, misemo na nahau nyingi.
 • Kubuni wahusika na mandhari: Mwandshi baada ya kujua kazi yake inahusu nini sasa inambidi abuni wahusika wa hadithi yake. Wahusika wanaweza kuwa ni watu, wanyama, mimea, mazimwi, malaika n.k. Pia ni lazima abaini mazingira ambamo visa vyote vya hadithi na matukio yatakapofanyika. Mandhari yanaweza kuwa baharini, kijijini, mjini, mbinguni, kuzimu n.k
 • Kupanga msuko wa visa na matukio: Msuko wa visa na matukio ni muhimu sana katika usimulizi wa hadithi. Sasa kama mwandishi amaeamua kuwasilisha kazi yake kwa njia ama ya hadithi fupi au riwaya au tamthiliya ni vema ajue namna visa na matukio vitakavyopangwa. Katika kufanya hivi maswali yafuatayo ni muongozo mzuri katika kupangilia ploti: Hadithi yangu itaanzaje? Mgogoro utaanzaje? Ni kati ya nani na nani? Je, kilele cha mgogoro ni nini? Je, ni mhusika mkuu kubakwa na kuambukizwa VVU? Hadithi yangu inaishaje? Je mhusika mkuu ashindwe? Atorokee nje ya nchi? Afungwe? Abadilike Au maadui ndio wafungwe au wafe? Au wabadilike?
 • Kuanza kuandika: Sasa baada ya kupitia hatua hizo zote, mwandishi sasa anaweza kuanza kuandika. Mchakato wa kuandika hua ni mrefu na mwandishi anaweza kujikuta anafuta mara nyingi kile alichokiandika, hii ni kutokana na kwamba mambo mengi ya kuandika huwa yanakuja wakati mwandishi ameanza kuandika kazi husika. Hata hvyo sio vibaya kufanya hivi, hii pia inasaidi kuwa na zao bora la fasihi.
Utungaji wa hadithi
Hadithi ni masimulizi ya kubuni yaliyoandikwa kinathari inaweza kuwa na wahusika wengi, matukio mengi na mandhari mapana (inategemena na aina ya hadithi, iwapo ni hadithi fupi wahusika wake huwa ni wachache na pia matukio ni machache, mandhari yake pia ni finyu). Kuna aina zifuatazo za hadithi kulingana na kigezo cha urefu au maudhui. Kwa kigezo cha urefu kuna Hadithi Fupi na Riwaya. Kutokana na maudhui kuna Riwaya Dhati na Riwaya Pendwa.
Riwaya dhati ni zile zinazozungumzia masuala muhimu ya kijamii, kama vile uonevu wa tabaka la chini, rushwa, uongozi mbovu n.k
Riwaya pendwa ni hadithi zenye lengo la kuburudisha, kutokana na usimuliaji wake uliojaa taharuki na fantasia. Mambo yanayosimuliwa katika riwaya hizi ni yale yanayogusa hisia za watu kwa urahisi kama vile mapenzi, mauaji, ujasusi n.k.

Mikondo ya uandishi wa hadithi
Mkondo wa hadithi ni mwelekeo ambao mwandishi anaufuata katika utunzi wa kazi yake. Mikondo ya utunzi wa hadithi ni pamoja na hii ifuatayo:
 1. Mkondo wa kiwasifu; mkondo huu huhusisha hadithi zote zinazosimulia maisha ya watu. Ni riwaya ambayo inasimulia maisha ya mtu toka alipozaliwa hadi wakati huo.
 2. Mkondo wa kitawasifu; hadithi zinazofuata mkundo huu ni zile zinazosimulia maisha ya mtu binafsi yaani mwandishi mwenyewe. Kwa mfano riwaya ya “maisha yangu baada ya Miaka hamsini”. (S.Robert)
 3. Mkondo wa kihistoria; hadithi katika mkondo huu zinahusu matukio ya kweli ya kihistoria yaliyotokea. Kwa mfano riwaya ya “Uhuru wa Watumwa”
 4. Mkondo wa kipelelezi; hizi ni hadithi zinazozungumzia upelelezi wa uhalifu fulani kama vile ujambazi, wizi, rushwa, mauaji n.k.
 5. Mkondo wa kimapenzi; katika mkondo huu zinaingia riwaya zote zinazozungumzia masuala ya mapenzi.
Utungaji wa hadithi fupi
Kama tulivyokwisha ona hapo nyuma sifa za hadithi fupi, basi katika utungaji wake mambo yafuatayo ni sharti yazingatiwe:
 1. Hadithi fupi inakuwa na mhusika mkuu mmoja ambaye anajitokeza sana kuliko wahusika wengine.
 2. Idadi ya wahusika ni ndogo ukilinganisha na wahusika wa kwenye riwaya.
 3. Mandhari ya hadithi fupi si mapana kama ilivyo katika riwaya
 4. Hadithi fupi inakuwa inaongelea dhamira kuu moja tu ambayo inaonekana toka mwanzo hadi mwisho wa hadithi.


                MADA YA SITA: ANDISHI WA INSHA NA MATANGAZO
Uandishi wa Insha za Kisanaa
Misingi ya Kuandika Insha
Insha za kisanaa ni insha zinazoelezea mambo ya kawaida katika jamii lakini kwa kutumia lugha ya kisanaa. Lugha ya kisanaa ni pamoja na matumizi ya tamathali za semi, misemo nahau, methali na taswira.
Muundo wa Insha
Kwa kawaida insha inakuwa na sehemu kuu nne: kichwa cha insha, utangulizi, kiini na hitimisho.
 1. Kichwa cha insha; Kichwa cha insha hudokeza kile utachokijadili katika insha yako, hubainisha wazo kuu la mada inayohusika. Kwa kawaida kichwa cha insha huandikwa kwa sentensi fupi. Mfano; maisha ya kijijini, mimba za utotoni.
 2. Utangulizi; Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako. Utangulizi unakuwa katika aya moja fupi.
 3. Kiini cha insha; Katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha yako, maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.
 4. Hitimisho; Hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichojadiliwa katika insha.
Insha za Kisanaa
Insha ya kisanaa ni ile inayotumia lugha ya kisanaa yaani yenye tamathali za semi kama vile sitiari, tashbiha, taniaba na mubalagha. Aidha insha ya kisanaa hutumia mbinu nyingine za kisanaa kama tashititi, takriri, na tanakali sauti. Vilevile insha za kisanaa huwa na lugha zenye mvuto na misemo kama nahau, methali na tamathali za semi.

Uandishi wa Matangazo
Tangazo ni taarifa za wazi zinazotoa ujumbe fulani kwa walengwa wanaohusika na ujumbe huo. Ujumbe unaweza kuwa na lengo la kushawishi, kuarifu, kuelekeza, na kadhalika.

Vipengele vya Kuzingatiwa katika Uandishi wa Mtangazo
Malengo ya matangazo
 • Kutoa taarifa;Lengo mojawapo la matangazo ni kutoa taarifa, mfano wa matangazo yanayotoa taarifa ni mialiko, tangazo la kifo, alama za barabarani, matangazo ya kazi.
 • Kuonya; Matangazo pia yana lengo la kuonya, kwa mfano matangazo kama vile ya kutovuta sigara, UKIMWI na kadhalika.
 • Kushawishi; Matangazo pia yana lengo la kushawishi, matangazo yenye lengo hili mara nyingi ni matangazo ya biashara ambayo kwa kweli lengo lake ni kushawishi wateja ili wanunue bidhaa zao, mtangazo ya mialiko hasahasa ya tukio fulani, labda msanii anazindua albamu fulani na kadhalika.
Jinsi ya kuandika matangazo
Ili tangazo liweze kufanikisha kufikia lengo lililokusudiwa kuna mambo kadhaa ya kufanya; mambo hayo ni kama yafuatayo:
 • Kichwa cha habari; Mara nyingi matangazo yanakuwa na kichwa cha habari, hii inasaidia kujua kwa haraka kuwa tangazo linahusika na kitu gani.
 • Kuonesha aina ya bidhaa/huduma; Hiki ndicho kiini cha tangazo, hapa tangazo linaonesha ujumbe uliokusudiwa kufikishwa kwa wahusika, sasa ujumbe huu waweza kuwa ni bidhaa inayotangazwa au huduma inayotolewa au kazi inayotangazwa au mwaliko unahusu nini.
 • Anwani; Hapa tangazo linaonesha mahali ambapo watoa tangazo walipo, yaani ofisi zao zilipo ambapo wahusika wa tangazo wanaweza kwenda na kuwakuta. Kama ni tangazo la mwaliko basi ni lazima lionesha shughuli yenyewe itafanyika wapi.
 • Njia za mawasiliano; Kama ni tangazo la biashara au la kazi au la mwaliko ni muhimu kutoa mawasiliano. Mawasiliano hayo yanaweza kuwa ni namba ya simu, fax, wavuti (kwa taarifa zaidi), barua pepe.
Mbinu za uandishi wa matangazo
Ili tangazo liweze kuvuta umakini wa watu ni lazima liwe na mwonekanao fulani. Zifuatazo ni mbinu za uandishi wa matangazo.
 • Matumizi ya picha; Matangazo mengi ya biashara huwa yanaambatana na picha, picha hizi hujaribu kumshawishi mteja aamini kuwa ile bidhaa ni bora na hivyo ni muhimu kuwa nayo au kuinunua.
 • Maneno machache; Matangazo hutumia maneno machache kwa lengo la kutomchosha mlengwa lakini wakati huohuo maneno hayo yana nguvu ya kumshawishi mlengwa.
 • Lugha ya kisanii; Maneno ya kisanii katika matangazo huwa ni mepesi kukumbukwa na huwa yanaeleweka kirahisi. Kwa mfano, matumizi ya vivumishi, litakuwa ni bonge la shoo, njoo ujinunulie pamba za ukweli, n.k. Matumizi ya mubalagha, kwa mfano; mtandao unaoongoza Tanzania, mganga bingwa afrika mashariki na kati n.k
 • Matumizi ya watu maarufu; Matangazo mengi hususani ya biashara hupenda kutumia watu maarufu ili kuwashawishi walengwa. Kwa mfano kama ni tangazo juu ya bidhaa fulani, huweza kumwonesha pengine msanii maarufu, miss Tanzania, au mchezajia mpira maarufu. Sasa mlengwa anapoona kwamba hata mtu maarufu anatumia hiyo bidhaa, anashawishika na yeye kuitumia


                            MADA YA SABA: KUSOMA KWA UFAHAMU
Kusoma Kimya
Ufahamu wa kusoma ni ule mtu anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu cha habari, kitabu au gazeti.

Maswali ya Ufahamu kutokana na Habari uliyosoma
Katika ufahamu wa kusoma, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
 • Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu inatkiwa ajiluze, Je, kinachoongelewa hapa nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi? Msomaji akiwa na maswali haya akilini mwake basi itakuwa rahisi kwake kuielewa habari hiyo.
 • Kuzingatia alama za uakifishi; msomaji ni lazima azingatie alama za uakifishi, kwa kufanya hivyo itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatazingatia alama za uakifishaji anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
 • Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, hii itamsaidia kuelewa vyema maana ya mwandishi.
 • Vilevile msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele anachokisoma inampasa akielewe vizuri.
Kwa kuzingatia haya yote msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma

Kufupisha habari
Kufupisha habari ni kuandika upya habari uliyoisoma kwa maneno machache lakini bila kupotosha ujumbe wa habari ya kwanza.
Ufupisho wa habari huwa na sifa hizi:
 • Huwa ni mfupi kuliko habari ya mwanzo
 • Huwa na ujumbe uleule uliokuwa katika habari ya mwanzo
 • Hujumuisha mawazo makuu yaliyodondolewa kutoka kwenye habari ya mwanzo
 • Mawazo haya sharti yapangwe katika mtririko wenye mantiki
Hatua za kufuata katika kuandika ufupisho
Ili kuweza kufanikiwa kufupisha habari kwa ufanisi hatua zifuatzo sharti zifuatwe:
 • Kuisoma au kuisilikiza habari kwa makini ili kuielewa vizuri
 • Kutambua na kubaini mawazo makuu yanayojitokeza katika kila aya
 • Kuyaunganisha mawazo makuu na kuandika au kuelezea ufupisho wa habari hiyo kwa maneno yako mwenyewe bila kupostosha maana ya habari ya kwanza.
 • Kuhesabu idadi ya maneno ya ufupisho ili kuyapunguza ikiwa yanazidi idadi iliyotakiwa.
 • Kama muda unaruhusu pitia tena habari ya mwanzo na pitia tena ufupisho ili kujiridhisha kuwa hujaacha taarifa yoyote ya muhimu.
Kufupisha Habari Uliyoisoma
Mtu mmoja na mkewe kutoka jamii ya Daliti inayobaguliwa tangu jadi nchini India wameuawa, mmoja akiwa amekatwa kichwa na mwengine kunyongwa kwa kushindwa kulipa deni la Rupee kumi na tano ambalo ni karibu senti ishirini na mbili tu.
Polisi kaskazini mwa taifa hilo wamethibitisha kisa hicho ambapo yasemekana mfanyi biashara anayetokea jamii ya hadhi ya juu,aliwaua wanandoa hao kwa kushindwa kulipa deni la biskuti walizokuwa wamewachukulia watoto wao.
Mfanyi biashara huyo amekamatwa.Ubaguzi kwa misingi ya kijamii umeenea sana nchini India, huku watu wa jamii ya Daliti waliokuwa wamebadikwa jina la 'the untouchables' wakiwekwa kwenye daraja la chini kabisa kwenye sera hiyo ya kibaguzi nchini India iitwayo 'caste' ambapo wananyimwa fursa nyingi za kimaendeleo na hivyo kubaki katika lindi la umaskini.
Hata hivyo Visa vya ukatili wa kibaguzi dhidi ya jamii ya Dalit katika jimbo la Gujarat vimeongezeka mnamo siku za hivi karibuni na vimesababisha wimbi la maandamano kutoka watu wa jamii hiyo.

Zoezi
Kwa maneno yasiyozidi 30 fupisha habari uliyoisoma hapo juu.GET NOTES THROUGH WHATSAPP/EMAIL BY PAYING LITTLE AMOUNT OF MONEY, CONTACT US 0759146185/ 0622105865

4 Comments

Post a Comment